VITA YA MAGHARIBI NA UCHINA KATIKA UWEKEZAJI AFRIKA
Ushirika wa China Afrika unaendelea kukua kwa kasi ya pekee na kuleta matumaini juu ya maendeleo katika nyanja zote. Hali hii imechangia mataifa ya magharibi kuingilia kati ushiriakiano hhuo na kutamka wazi una lengo la kuitawala Afrika .
Halikadhalika katika miaka mingi ambayo serikali ya jamuhuri ya watu china imekuwa ikikita mizizi ya uwekezaji katika nchi zsa kiafrika ambao kwa hali inavyoonekana ni ya kutia moyo kwani wamewekeza zaidi katika huduma za jamii na misaada isiyo na masharti makali kama nchi zqa magahribi.
Inavyoaminika kuna zaidi ya makampuni 800 ya kichina yanayo fanya shughuli mbambali za kiuchumi na kijamiii katika Afika hususani miundo mbinu, taasisis za fedha vileveli nishati, katika uwekezaji huu na biashara uchina inayofanya na Afrika huweka masharti nafuu ambayo kwea ujumla huwa ni mabadilishano kwa ujenzi wa miundo mbinu na misaada isiyo na masharti magumu.
Kwa mujibu wa wataalamu msimamo wa China wa kutoingilia kati masuala ya ndani ya Afrika umepelekea bara hilo kujipatia misaada ya fedha inayoihitaji mno bila ya kuwekewa masharti ambayo baadhi ya mataifa ya magharibi huyaweka wakati wa kutowa mikopo kwa Afrika. Msimamo huo wa China umechangia ujenzi wa haraka wa miradi ya miundo mbinu barani humo.
Licha ya kuwa na mahusiano na uwekezaji wenye tija kwa nchi za kiafrika bado kuna tetesi kutoka kwa baadhi ya wasomi na vyombo vya habari vya nchi za magharibi kuwa mapandikizi ya udikteta katika baaadhi ya nchi za kiafrika ni uzao halali wa uwekezaji namahusiano ya kibiashara baina ya china Afrika na kutolea mfano nchi kama Zimbabwe na Rwanda.
Hivyo tafsiri hii inatia shaka kwa uwekezaji nchi hizo za magahribu zinavyootaka ukue na nchi za kiafirka ambao tahadhari zake hazijawekwa bayana. Katika taarifa iliyotolewa na BBC mwaka jana ilitamka wazi ya kwamba, China hufanya shughuli zake kivyake sio kama kanda bali nchi hiyo inaendeshwa na waekezaji wa binasfi, mashirika ya kiserikali na wafanyabiasha wachina walio barani Afarika na ambao hushindana wenyewe ka wenyewe pasipo kujali kauli mbiu ya taifa hilo la kikomunisti.
Vita hivi vya uchina na magharibi vinaendelea ambapo waafrika wengi wanategemea zaidi bidhaa na huduma pamoja na misaada kutoka china na sio nchi za magharibi kwani huwsa zina masharti ambayio ni magumu. Kama alivyowahai kutamka waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon katika mkutano wa jumuiya ya madola juu ya misaada na tabia za ushoga wakati wachina ni misaada na uwekazaji katika viwanda na biashara.